30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari ya Dar es Salaam imemuingiza Rais Samia kwenye vita ya kiuchumi

Na Thadei Ole Mushi

Chukua kalamu na karatasi kwenye andiko hili unaweza kuandika chochote…. Ipo hivi….

Bandari ya Daresalam inahusika kwa asilimia 95% kwenye biashara za Kimataifa Tanzania. Ni eneo Muhimu mno na fursa kubwa sana kwa nchi yetu. Ukiigusa Bandari yetu kwa jema au baya basi umegusa asilimia 95 za biashara kati ya Tanzania na maeneo Mengine.

Kupitia rank za World Bank’s Conteiner Port Performance index (CPPI) inaonyesha mwaka 2022 Bandari ya Daresalam ilishika nafasi ya 361 kati ya Bandari 386 kwenye utoaji wa huduma za kibandari Duniani. Mwaka wa 2023 tukashika nafasi ya 312 kati ya bandari 348. Tafsiri yake ni kwamba bado Bandari yetu haifanyi vizuri hata kidogo pamoja na kwamba inatajwa kuwa ipo eneo zuri kuliko bandari Nyingi Duniani.

Kwa mfano mwaka 2021 World bank walitoa ripoti ya CPPI (Global ranking of container Ports) ambapo Bandari ya Daresalam ilishika nafasi ya 361 kwa ubora kati ya bandari 379 zilizoorodheshwa, yaani tulikuwa ni wa 9 kutoka Chini. Kwenye kipengele cha administrative approach bandari yetu ilikuwa na points negative -248 na katika kipengele cha Statistical approach tulikuwa na points negative -105. Tafsiri ya hizi negative ni kwamba Bandari yetu uongozi ni Mbovu, kupita kiasi na utendaji wake kwa ujumla ni mbovu kupita kiasi hivyo Bandari yetu inafanya kazi Chini ya kiwango na katika udhaifu mkubwa. Nakuwekea link kabisa uweze kupitia ripoti hiyo ya worl Bank:- https://thedocs.worldbank.org/en/doc/66e3aa5c3be4647addd01845ce353992-0190062022/original/Container-Port-Performance-Index-2021.pdf

Kutokana na Kufanya huko vibaya nchi ambazo tulikuwa tukizihudumia zimeshaanza kutuhama hivyo kunahitajika juhudi za makusudi na za haraka kabisa kuponyesha bandari yetu kutokana na umuhimu wake kwenye uchumi wetu.

Wataalamu wanasema kutokana na hali ya Utulivu ya Tanzania kisiasa,na kijamii Bandari ya Daresalam imeendelea kuwa Chaguo la kwanza kwa nchi zote ambazo hazina bandari na tumepakana nazo. Bandari ya Daresalam imeendelea kuwa chaguo la Kwanza kwa nchi za Zambia, DRC, Malawi, Burundi, Rwanda na Uganda. Kwa sasa nchi hizi zimeanza kufikiria kuchukua Risk za kibiashara kupitisha mizigo yao kwenye Bandari za Mombasa, na Durban Africa Kusini kutokana na Huduma mbovu kwenye Bandari yetu. Tukicheza washindani wetu wataua kabisa Uchumi wetu hivyo hili jambo lazima tulijadili tukiwa tumetanguliza Uzalendo mbele bila kuwa na interest zozote zile.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kwenye Bandari kumi bora Dunian taifa la China linaingiza Bandari zake saba kwenye top ten. Lakini ukifuatilia kwa nini China wanafanya Vizuri sana kwenye mambo ya Bandari utagundua kwamba katika Bandari zake tano ambazo zipo kwenye top ten ya Dunia anayeziongoza ni Mwekezaji toka nje. Sio kwamba China imeshindwa kuongoza ila kampa mwenye uzoefu zaidi hizi rasilimali za Dunia huwezi kuzifaidi zote kwa kuzikalia mwenyewe…. Wewe una dhahabu lakini huna Technolojia lazima ukubali kubadilishana ili nyote mnufaike.

APM terminals kampuni ambalo ni subsidiary ya kampuni Maersk toka Denmark ndio waliowekeza kwenye hizo bandari za China. Zaidi ya asilimia 50 ya uendeshaji wa bandari za China zinaendeshwa na makampuni ya nje (Wawekezaji). Kuna haja ya kutafakari sana wakati tukiendelea na mjadala huu wa Bandari kuwa issue si mkataba tu kukosewa ila ndani yake pia kuna Vita kubwa ya Kiuchumi.

Kwenye hili la Bandari Rais Samia ni Dhahiri ameingia kwenye Viunga vya Uwanja wa Vita ya Kiuchumi hili linaonekana wazi wazi kwa sasa. Tulizoea kumsikia Rais Magufuli akisema vita ya Kiuchumi ni Ngumu hatukuwa tunamwelewa. Ndio maana alivyoanza ujenzi wa Miradi Miwili Mikuwa wa Umeme na SGR ndio kipindi alichopigwa vita kuliko kipindi kingine nje na ndani ya Nchi. Na katika kipindi alichokaa madarakani SSH kama Rais wa Nchi wakati huu wa uwekezaji wa Bandari ndio wakati ambao kelele na kurushiwa mawe kumeongezeka.

Ukiachana na Bandari SGR nayo ilikuwa ni vita…..

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Sehemu ya kipande cha Reli ya Kisasa (SGR) .

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

“Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika….

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Dar es Salam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC – The East African – https://www.theeastafrican.co.ke/business/Tanzania-signs-mega-sgr-deal-with-burundi-drc/2560-5377324-75ujpd/index.html

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.

Vita nyingine ya kiuchumi ilikuwa Stiglers…

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga. Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira….

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais Magufuli. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.

https://www.lifegate.com/people/lifestyle/stieglers-gorge-dam-tanzania

Stiglers itatuondoa kabisa kwenye uhaba wa umeme na kutufikisha kwenye Uchumi wa viwanda. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa jirani ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda..

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?…..

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Kwa maana hiyo hili la bandari Vipengele vya Mkataba vinatumika tu kama Silaha ya kupigana vita hii…. Tuangalie panapofaa kurekebisha tukamilishe hili dili haraka sana tumechelewa. Tumuunge mkoni Rais katika nia yake njema hii.

Share kwa manufaa ya taifa lako…..

Ole Mushi
0712702602

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles