24.3 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

PURA, DC Mtwara wafanya mazungumzo kuhusu CSR

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imefanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha kujadili uandaaji wa Mwongozo wa uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibility – CSR Guidelines) ambao utasaidia utekelezaji wa miradi ya CSR inayofanywa na kampuni za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini.

Mazungumzo hayo yalifanyika Julai 20, mwaka huu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Wakurugenzi wa Hamlashauri za Manispaa za Mtwara mjini na vijijini na wataalamu kutoka PURA na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandihi Charles Sangweni amesema kuwa chimbuko la kuandaliwa kwa Mwongozo wa uwajibikaji wa kampuni kwa jamii ni Kifungu Namba 222(4) cha Sheria ya Petroli ya Mwaka 2015 na kwamba ni wakati muafaka sasa kuweka mwongozo utakaowezesha utekelezaji wa miradi ya CSR inayozingatia mahitaji na vipaumbele vya jamii.

“Sisi kama PURA wakati mwingine tunapozunguka kukagua utekelezaji wa miradi ya CSR na kuhoji uongozi wa jamii husika kama ulishirikishwa katika kupanga aina ya mradi wa kutekeleza, tunakuta kwamba baadhi ya miradi haikuzingatia vipaumbele vya jamii husika, hali inayopelekea mradi kutelekezwa au kutokutumiwa kulingana na matarajio,” amesema Sangweni.

Nae Mkuu wa Wilaya hiyo Hanafi alieleza kuwa na Mwongozo huo ni muhimu na kuipongeza PURA kwa kuchukua hatua ya kuchagiza uaandaaji wa Mwongozo huo.

“Ombi langu kuu ni kwamba Muongozo huo wa CSR ujumuishe namna ya kukokotoa kiasi ambacho kampuni zitatakiwa kuchangia katika miradi ya CSR kwani kwa sasa hakuna fomula maalum ya kukokotoa kila kampuni ichangie vipi kulingana na faida inayotengeneza au ukubwa wa uwekezaji,” aliongeza Hanafi.

Aidha alitoa pendekezo la kuwa na fomula maalum, Hanafi aliomba pia, kama itawezekana, kuwepo kwa mwongozo mmoja kwa sekta zote kwani CSR sio kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles