23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

BALOZI ‘CISCO’ MTIRO AZIKWA KISUTU DAR

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally, akiongoza swala ya kumwombea dua aliyekuwa Mkuu wa Itifaki mstaafu marehemu Balozi Abdulkarim Mtiro “Cisco” nyumbani kwake Mikocheni B, Dar es Salaam jana kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Kisutu jana. Picha na Deus Mhagale.

 

 

ASHA BANI na LEORNAD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

MARAIS Wastaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi wa awamu ya pili na Jakaya Kikwete wa awamu ya nne, jana waliongoza mazishi ya aliyekuwa mkuu wa Itifaki, Balozi Abdulkarim  Mtiro ‘Cisco’.

Alizikwa  jana katika makaburi ya Kisutu,  Dar es Salaam, ambako mamia ya wanasiasa na watu maarufu walihudhuria. 

Balozi  Mtiro alifariki Juni 5 , mwaka huu katika Hospitali ya Aghakhan.

Akisoma wasifu wa marehemu,   ndugu wa Balozi huyo, Said Ibrahimu alisema ‘Cisco’ alikuwa   mtu wa watu aliyependwa na kila mtu.

Alisema  alizaliwa Novemba 25, mwaka 1950 Gerezani Kariakoo na baadaye kuhamia Temeke alikoanza shule ya msingi.

Ibrahimu alisema ‘Cisco’ alifaulu masomo yake ya darasa la saba na kujiunga na sekondari ya Agakhan Boys kabla  ya kujiunga na Chuo cha Biashara (CBE) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Baadaye  aliajiriwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ambako alifanya kazi katika idara mbalimbali.

“Baadaye alikuwa Mkuu wa Itifaki   ambako aliweza kuhudhuria na kuongoza mikutano mbalimbali ikiwa ni pamoja na   mapokezi ya Rais wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela ‘Madiba’ na kuandaa mkutano mkubwa wa kwanza wa Jumuia ya Madola.

“Baadaye alichaguliwa kuwa balozi  katika nchi mbalimbali   kabla ya kurejea nchini,’’ alisema Ibrahimu.

Marehemu ameacha mke na watoto wane, wa kike watatu na mmoja wa kiume.

Balozi Cisco   pia aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia na Singapore

 Akitoa salamu za rambirambi katika msiba huo,  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zubeir, alisema ni msiba mkubwa kwa watu wote na kwamba ni mambo ya Mungu ambaye ameamua kumwita ‘Cisco’.

Alisema kufa ni lazima kwa kila mtu kwa kuwa ni utaratibu na kila mmoja atarudi katika njia hiyo hiyo..

Sheikh  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salum alisema mauti siyo mwisho wa maisha.

Alisema anaamini kuna maisha baada ya kufa  na kwamba adhabu ya kaburi ipo na neema pia ipo.

 Mbali na marais wastaafu,  viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na  aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Alhaji Adam Kimbisa.

Wengine ni Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,  Ramadhan Madabida, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete, Balozi Juma Mwapachu na viongozi wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles