26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Baba wa Beyonce alimhofia R. Kelly

NEW YORK, MAREKANI

BABA wa Beyonce, Mathew Knowles, ameweka wazi kuwa alikuwa makini kumlinda mwanawe huyo na Kelly Rowland, wakati wanafanya kazi na staa wa muziki wa RnB, R. Kelly.

Knowles ambaye alikuwa meneja kwenye tasnia ya muziki, aliwahi kufanya kazi na R. Kelly mwaka 1998, huku Beyonce na Kelly Rowland wakiwa na umri wa miaka 17.

“Nilikuwa makini sana wakati nafanya kazi na R. Kelly, ilikuwa mwaka 1998, wakati warembo hao wakiwa na umri wa miaka 17, sikutaka kuwaacha peke yao, mara zote nilikuwa namwambia mke wangu Tina aungane nao kokote aendako hata kama bafuni kuliko kuwaacha wakiwa na R. Kelly.

“Kwa kufanya hivyo, warembo hao walikuwa sehemu salama, muda mwingi nilikuwa nao studio huku nikiwa na R. Kelly, lakini hakuweza kufanya lolote,” alisema Knowles.

R. Kelly kwa sasa yupo katika wakati mgumu kutokana na kashfa zake za unyanyasaji wa kingono.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles