24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Kundi la Rostamu lajivunia idadi kubwa ya mashabiki

JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kizazi kipya na kundi la Rostamu, Stamina, amesema muunganiko wao na Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, umewaongezea idadi kubwa ya mashabiki ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Stamina alisema awali kila mmoja alipokuwa akifanya kazi zake binafsi, walikuwa na mashabiki, lakini wakati huu hali imebadilika wameongezeka zaidi ya matarajio yao.

Alisema hakuna kazi ya pamoja waliyofanya haijawahi kupokelewa vema na mashabiki, kila wimbo unapotoka lazima ukubalike.

“Tunashukuru sana, kazi zetu za pamoja zimeweza kutuongezea idadi ya mashabiki na kufanya vizuri sokoni tofauti na matarajio yetu,” alisema Stamina. Stamina alisema wamejipanga kufanya kazi nyingi zaidi kadiri watakapokuwa wakipata nafasi, ila hata pale watakapo lazima kutoa kazi binafsi watafanya pia

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles