25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

B Bonics aachia ‘Free Style’ mpya

GEORGIA, MAREKANI

KUTOKA Atlanta Georgia, Marekani, rapa anayekuja kwa kasi, B Bonics, amewaomba wapenzi wa Hip hop kuitafuta ngoma yake mpya, Fee Style inayopatikana kwenye mitandao yote ya muziki.

Akizungumza na MTANZANIA, Bonics mwenye asili ya Ghana, alisema Fee Stle hiyo ni mwanzo mzuri wa lebo yake, Living Large Entertainment kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa Hip hop.

“Nimeanza lebo ya Living Large Entertainment ili kusukuma zaidi harakati za Hip hop hasa za kumkomboa mtu mweusi. Fee Style ndio ngoma yangu mpya ya kuhakikisha nafanikisha ndoto hizo, wimbo tayari upo YouTube na ngoma nyingine kama Yi Weni, Ohemaa, Yaabi, Kwame Nkrumah (Genius) na Superstar,” alisema Bonics.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles