Msafiri Tunga aiweka wazi ‘Wastahili Bwana’

0
604

PHOENIX,MAREKANI

SIKU chache baada ya kuachia, Rafiki Mwema, mwimbaji wa Injili anayeishi Phoenix, Marekani, Msafiri Tunga, amewaomba wapenzi wa muziki huo kuipokea tena video ya wimbo wake, Wastahili Bwana aliomshirikisha Stephano Iddy.

Tunga ameliambia MTANZANIA kuwa wimbo huo ni wa kusifu na kumwabufu Mungu na mtu yeyote anaweza kuusikiliza na akapata ujumbe utakaoimarisha uhusiano wake na Mungu.

“Nimeachia video mpya, Wastahili Bwana ambayo tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube (Tunga MSK), wimbo huu una mguso wa kipekee sana naamini wengi watabarikiwa,” alisema Tunga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here