24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Azam wapigia hesabu pointi tatu za Coastal

Theresia Gasper -Dar es salaam

BAADA ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, Uongozi wa Klabu ya Azam, umesema nguvu zao wanazielekeza kwenye mchezo wao unaofuata dhidi ya Coastal Union.

Azam itakuwa mwenyeji wa Coastal, katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bata utakaochezwa Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam.

Miamba hiyo ya soka yenye maskani yao Chamazi nje ya nje ya Dar es Salaam itawavaa Coastal, ikitoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Kwa upande wake Coastal itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoa suluhu dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa jana.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Jafar Idd, alisema kwa sasa wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo wakiwa na kiu ya kutaka kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza.

“Baada ya ushindi wa jana (juzi), timu itaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union, kwani mara ya mwisho tulivyokutana nao katika uwanja wao walitufunga 1-0,” alisema.

Alisema wachezaji wote wapo vizuri kwa sasa na hakuna majeruhi hivyo benchi la ufundi litaendelea kukinoa vema kikosi ili waendeleze kupata matokeo mazuri.

Idd alisema hawapo tayari kuona wanapoteza mchezo tena kwa Coastal Union, hivyo umakini mkubwa unahitajika kuhakikisha pointi tatu muhimu zinasalia nyumbani.

Azam FC wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakijikusanyia pointi 44 kati ya michezo 21 walizocheza wakishinda mechi 13 sare zikiwa tano huku wakipoteza mara tatu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles