30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Azam waikatalia ubingwa Simba

ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa Azam, Idd Nassoro ‘Cheche’, amesema hawajakata tamaa katika harakati ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Cheche alisema licha ya Simba kuonekana kutangulia mguu mmoja katika mbio za kutetea ubingwa wao wanaendelea na mapambano ya kuwania taji hilo.

Cheche alisema pamoja na  kuzidiwa alama nyingi na Simba walio juu yao katika msimamo lakini wanaamini wana nafasi ya kutwaa ubingwa.

 “Simba wmaetuzidi alama 14 ambazo ni sawa kama na michezo mitano, hatujakata tama tunanafasi ya kutwaa ubingwa wa msimu huu kwa sababu  waliojuu yetu wanaweza kupoteza mechi.

“Ligi ni ngumu kila mtu anapambana  sitaki kuamini kuwa mechi walizobaki nazo Simba watashinda zote, kwa sababu timu nyingi wanazokutana nazo zipo katika hatari ya kushuka daraja najua haziwezi kukubali kupoteza kirahisi na hiyo ndio nafasi yetu ya kuchukua kombe.”

Azam ambayo ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 45, baada ya kucheza mechi 23 sawa na Simba,  lakini wakizidiwa kwa alama 14 baada ya Wekundu wa Msimbazi kujikusanyia 62.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles