27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Kitayosa yaitahadharisha Ndanda FC

GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Kitayosa, Boniface Kiwale, amesema kikosi chake hakina hofu hivyo watapambana kufa au kupona dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Kombe la FA utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Kitayosce ilitinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya kuiondoa Lipuli kwa mikwaju ya penalti 5-4 kutokana na sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo huo, wakati Ndanda ikiitoa Dodoma Jiji kwa mabao 2-0.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kiwale alisema wanatambua wanakutana na timu yenye uzoefu, wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanaitoa Ndanda kwenye michuano hiyo na kuzidi kusonga mbele.

Kiwale alisema amefanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika mchezo uliopita, hasa safu ya ulinzi ambayo ilifanya uzembe na kusababisha wapinzani wao Lipuli kusawazisha bao na kutoka sare ya 1-1 kabla ya kuingia hatua ya penalti.

“Tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo mazuri japokuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini tutapambana kufa au kupona kuhakikisha tunatinga hatua inayofuata.

“Nimeiona siku za karibuni Ndanda, wamekuwa wakifanya vizuri kwenye Ligi Kuu hasa kwa michezo yao mitano iliyopita, lakini hilo halituogopeshi zaidi ya kwamba tunajipanga kupambana ili tuweze kushinda,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles