30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

‘AZAM ILIKUWA NA TATIZO LA STRAIKA, MAWINGA’

 Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche, amesema kikosi chao kilikuwa na mapungufu katika safu ya ushambuliaji na mawinga, katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu hiyo imefanikiwa kumaliza ikiwa katika nafasi ya pili ikijikusanyia pointi 58

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cheche, alisema timu yao ilijitahidi na kufanikiwa kumaliza ikiwa katika nafasi hiyo, hivyo lazima msimu ujao waje kivingine.

“Mapungufu yalionekana katika safu ya ushambuliaji ikiwa pamoja na winga, lakini sehemu nyingine zilikuwa vizuri hivyo naamini msimu ujao tutakuwa vizuri zaidi,” alisema.

Alisema licha ya kushindwa kutwaa taji la Ligi Kuu msimu huu na kumaliza nafasi ya pili, malengo yao ilikuwa ni kutengeneza kikosi lakini msimu ujao watakuja wakiwa na nguvu mpya.

Cheche alisema kuna wakati kikosi chao kilikuwa kikipata matokeo yasiyoridhisha na kuwakatisha tamaa mashabiki wao, lakini walipambana na kufikia hapo walipo sasa.

“Ligi ilikuwa ni ya ushindani mkubwa ukiangalia kila timu ilikuwa ikipambana ili kuweza kupata matokeo mazuri, lakini mwisho wa siku bingwa alipatikana hivyo tunajipanga kwa msimu ujao,” alisema.

Akizungumzia ujio wa Donald Ngoma katika kikosi hicho, alisema kwa sasa hawawezi kumzungumzia hadi hapo atakapoanza kucheza.

Timu hiyo kwa sasa imeenda mapumziko baada ya ligi kumalizika hadi hapo Julai 3, mwaka huu na kuanza mchaka mchaka wa maandalizi ya msimu ujao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles