25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Atupwa jela kwa kujaribu kujiua

Twalad Salum – Mwanza

MKAZI wa Kijiji cha Usagara, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Dementilia Saidia (22), amehukumiwa kifungo cha nje miezi mitatu kwa kujaribu kujiua kwa kujinyonga kwa kitenge.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, Eric Marley, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Ramsoney Salehe alidai kuwa mtuhumiwa huyo alijaribu kujiua kwa kutumia kipande cha kitenge.

Alisema katika Kijiji cha Usagara saa 7 mchana Januari 28, mwaka huu, mshtakiwa Dementilia Saidia, akiwa ni mtumishi wa ndani kwa Melesiana Marco (35) alijaribu kujinyonga na kujifunga kitenge shingoni na kujining’iniza jikoni kwenye kenchi na kuokolewa, kinyume cha sheria kifungu cha 217 kujaribu kujiua sura ya 16.

Baada ya mtuhumiwa kusomewa shtaka, Hakimu Marley alimuuliza kama ni kweli tuhuma hiyo, na alikiri kutenda kosa hilo baada ya mwajiri wake kumfukuza alipobainika kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu na aliyempachika aliikataa.

“Nilichangayikiwa nikaona nijinyonge kwani mwajiri ananifukuza nyumbani na aliyenipa mimba ananikataa,” alisema Dementilia.

Mahakama baada ya kumsikiliza mtuhumiwa kwa kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu na ukubwa wa tatizo ilimfunga kifungo cha nje miezi mitatu na kipindi chote atakuwa chini ya maofisa Ustawi wa Jmaii kwa uangalizi wa karibu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles