23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ATEMBEA KWA KUTUMIA MIKONO BADALA YA MIGUU

UKIISOMA simulizi hii au kuangalia picha unaweza kudhani ni mazoezi ya kawaida kama unayoyaona mitaani au ‘hobby’ tu ya mtu anayependa kufanya zoezi la kutembea kwa mikono.

Kuna watu wengi wenye uwezo wa kufanya hivyo kama sehemu ya mazoezi au ‘hobby’ tena isiyochukua muda mwingi, lakini kwa Dirar Abohoy ni hali tofauti, kwani ndiyo staili yake ya maisha halisi.

Kwamba licha ya kuwa na miguu kamili isiyo na tatizo lolote, badala ya kuitumia, yeye hutumia sehemu kubwa ya maisha yake kutembea kwa mikono.

Mkazi huyo wa Tigray, kaskazini mwa Ethiopia mwenye umri wa miaka 36, amekuwa akitembea kwa kutumia mikono tangu akiwa mtoto.

Amekuwa akitumia zaidi ya saa sita kutembea kwa mikono, kitendo ambacho hata hivyo, si kila mtu anakishabikia.

Kamwe hakuwahi kujaribu kutumia miguu yake, ametumia miaka yake 30 ya kwanza ya maisha yake kutembea kwa mikono yake badala ya miguu.

Ni kwa sababu alikuwa na mtazamo hasi kwamba kutembea kwa mikono ni rahisi zaidi na hufanya maisha kuwa rahisi kuliko miguu na kwamba ni njia nzuri ya kusafiria.

Abohoy huweza kutembea kwa mikono mahali popote pale sawa na mtu anayeitumia miguu kutembea au kuishi.

Huitumia mikono bila matatizo badala ya miguu kupanda na kushuka mlimani, kupanda au kushuka ngazi, kubeba vyuma vizito.

Kadhalika huendesha ngamia kwa kutumia mikono miguu ikiwa juu, humbemba mtu hata kuvuta au kusukuma gari akitembea kwa mikono.

Hali kadhalika huwa kivutio anaposafiri katika gari akiwa juu ya bodi, amesimama kwa mikono.

Anasema alianza kutembea kwa mikono akiwa na umri wa miaka tisa. Lakini pia ilikuaje akachagua staili hiyo ya maisha, ambayo kwa wengine ni kama mateso?

Anasema akiwa mdogo alizoea kuona filamu za Kichina au Marekani zikionesha watu wakitembea kihivyo.

Naye kwa akili yake ya kitoto iliyokuja kukomaa akadhani wanachofanya ni kitu cha kweli, yaani ndiyo maisha halisi wanayoishi watu hao.

Kwamba kile kinachoonekana katika filamu hizo ikiwamo kutembea kwa mikono ni kitu halisi na cha kweli.

“Sikujua kuwa kinachoonekana katika filamu ni mchezo uliohaririwa kwa kompyuta,” anasema na kuongeza:

“Wakati ninapotembea kwa mikono watu hawaamini kama ninafanya hivi kiukweli. Kwao wanadhani naigiza au kufanya onesho au ama kama sehemu ya ‘hobby’ yangu, wengine wanadhani ni uchawi au mazingaombwe!” anasema.

Kila siku natembea hivi kwa saa sita; yaani asubuhi saa tatu na jioni saa tatu.

Kwa Dirar, kusafiri kwa mikono miwili ilikuwa ni rahisi sawa na kutembea kwa miguu miwili.

Sikutarajia kuwa nitaacha kufanya nifanyavyo, nataka kuingia katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records.

Lakini si kila mtu yu mshabiki wa anachokifanya.

Mama yake Gidey Negash anasema ana hofu mwanae siku moja atavunjika shingo au kuangukia milimani wakati akiwa peke yake

Pamoja na majaribio mengi ya kumshawishi atembee kwa miguu yake, ushawishi uliofanywa na ndugu, jamaa kwa marafiki kwa miaka mingi, aligoma kuachana na staili hiyo, akisema ni njia nzuri zaidi kwake kuishi.

Dirar alikuwa na wasiwasi kubadili mwenendo huo kungeyafanya maisha kuwa mabaya, akiamini kutembea kwa mikono ni rahisi na bora zaidi.

Familia yangu hainiungi mkono ninachofanya lakini watu wengine hunitia moyo kuendelea,” anasema.

Haijalishi iwapo ninakula au la, lakini najua siwezi kuishi bila kufanya hivi, hakuna kitu kingine kinachoweza kuniridhisha na kunifurahisha zaidi ya hiki.

Shukrani kwa ushawishi uliofanywa bila kuchoka na watu waliomjali na kumpenda ndugu kwa marafiki, hatimaye Dinar aliweza kuachana na matumizi ya mikono kutembea.

Kwa sasa anafanya kama mazoezi au hobby tu. Na anakiri kinyume na alivyokuwa akifikiria awali kwa sasa maisha yake yamebadilika tangu aanze kutumia miguu kusafiria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles