31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ZUMA KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI


RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Durban leo akikabiliwa na mashitaka 16 ya ufisadi.

Mashitaka hayo yanahusiana na mkataba wa mauzo ya silaha, moja ya kashfa zilizomuandama kwa kiwango kikubwa wakati akiwa madarakani.

Kashfa hizo pamoja na utawala mbovu ulioshuhudia uchumi ukiporomoka ndizo zilizoshusha umaarufu wa Zuma na ANC ambacho kulimuondoa madarakani Februari mwaka huu.

Zuma atafika katika Mahakama Kuu ya Durban iliyoko kwenye jimbo lake la nyumbani la KwaZulu-Natal, kwa ajili ya hatua ya awali ya shauri hilo ambalo linaweza kumpeleka jela.

Makundi ya wafuasi wa Zuma pamoja na wapinzani wake kisiasa wanatarajiwa kuandamana nje ya mahakama.

Inatarajiwa ulinzi kuwa mkali mahakamani hapo ili kuzuia uwezekano wa vurugu kutokea.

Zuma anatuhumiwa kupokea rushwa ya Dola za Marekani bilioni tano kutoka Kampuni ya Kutengeneza Silaha ya Ufaransa ya Thales alipokuwa waziri wa uchumi na Naibu Rais wa ANC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles