29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

ATCL yatajwa kuendelea kupata hasara

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023, imeonesha Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imeendelea kupata hasara kwa miaka sita mfululizo.

Akiwasilisha ripoti hiyo Aprili 15,2024 mbele ya waandishi wa habari,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG),Charles Kichere amesema mashirika yasiyo ya kibiashara yaliripoti nakisi kutokana na upungufu wa fedha kutoka Serikalini na vyanzo mbadala vya mapato.

Ripoti hiyo iliwasilishwa Machi 28,2024 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino na mapema jana imewasilishwa Bungeni na Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande kisha baadaye CAG kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo imeonesha mashirika ya umma 24 yaliyopata faida au ziada katika mwaka wa fedha 2021/22, yamepata hasara au nakisi katika mwaka wa ukaguzi wa 2022/23 ATCL imeendelea kupata hasara kwa miaka sita mfululizo.

CAG amesema mwaka wa fedha wa 2022/23 kampuni hiyo ilipata hasara ya shilingi bilioni 56.64.

“Hasara hii imeongezeka ikilinganishwa
na hasara ya shilingi bilioni 35.23 mwaka wa 2021/22, ATCL imeendelea kupata hasara licha ya kuwa inapokea ruzuku kutoka Serikalini,”amesema CAG.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles