28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara kutafuta njia uboreshaji vibali vya biashara ya nyama

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema wanaangalia namna bora ya utoaji wa vibali kwa wafanyabiashara wa nyama na uvuvi ili wafanye shughuli zao popote Tanzania Bara na Zanzibar.

Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 17,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Ulega amesema haiwezekani mtu akitaka kufanya biashara ya nyama Visiwani Zanzibar kuwe na vikwazo vingi.

“Tumeanza kulijadili hili lazima mtu afanye biashara kwa uhuru, nawashukuru wataalamu kwa kuanza hili nina uhakika tutapata majawabu,”amesema Ulega

Kuhusu vibali vya uvuvi amesema “Zanzibar ukipata leseni haifanyi kazi tuna leseni mbili tofauti hili tunalitafutia dawa na linaenda vizuri. Hili jambo tunalitafakari kwa umakini.Tunataka mtu avue kutoka Dar mpaka Pemba ili kuwe na maana pana ya kukuza uchumi,”

Akizungumzia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji amesema wizara imeanza kugawa mbegu kwa ajili ya kupatikana kwa malisho bora kwa wafugaji.

Kuhusu uuzaji wa nyama nje ya Tanzania Waziri Ulega amesema soko la nje limefunguka hivyo watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles