29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Askofu Dk.Shoo: Chagueni viongozi waadilifu, wenye kuchukia rushwa

Na Mwandishi wetu- Arusha

ASKOFI Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi  ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro,Dk.Fredrick Shoo amewataka viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuwahamasisha waumini wao kuombea uchaguzi mkuu pamoja na kuchagua viongozi wenye uadilifu wenye kuchukia vitendo vya rushwa.

Akizungumza wakati wa ibada ya kumstaafisha msaidizi wa askofu, Mchungaji Paulo Urio,Dk.Shoo alisema kuelekea  uchaguzi mkuu, ni vema watu wakachagua viongozi waadilifu wenye hofu ya Mungu na wanaochukia rushwa.

“Nitumie fursa hii kuwasihi wa wakristo na Watanzania kwa ujumla ili muweze kuchagua kiongozi wenye sifa ambao watakuwa wa kwanza kupiga vita vitendo vya rushwa kwa kujitokeza kwenye kampeni zinazofanywa na vyama mbalimbali kusikiliza sera zao,nanyi wakristo kwa nafasi yenu napaswa mkatae rushwa kwa namna yeyote ile na msikubali kutumiwa na watu kwa manufaa yo,”alisema.

Aliwataka wakristo kuendelea kumtegemea Mungu, na si kutumia akili zao wenyewe, huku wakifahamu ndani ya kristo ni familia moja.

Aliwataka viongozi na waumini wote kuona umuhimu wa kujua msingi wa imani yao kuisimamia kuwaongoza watu, kwani wakristo wengi hawana ufahamu wa kutosha katika kile wanachokiamini ndiyo maana imani zao zinatikishwa kila wakati.

Akifungua Mkutano Mkuu wa 14 wa Dayosisi ya Meru uliofanyila Chuo Kikuu cha Makumira, Askofu wa Dayosisi ya Meru, Mchungaji Elias Kitoi aliweataka wajumbe wa mkutano huo kudumisha umoja walionao kwa mafanikio ya dayosisi na jimbo kwa ujumla.

“Tushirikini mkutano huu mkuu kwa kutoa mawazo chanya ya kwenda mbele, ni imani mkutano huu utawaimarisha,utawatuliza na utakuwa mkutano wa kiroho ili mkazidi sana kuitenda kazi ya bwana siku zote mkijua ya kwamba taabu yenu si bure katika bwana maana yeye atawafikisha salama,”alisema.

Akitoa salamu kwa  niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Iddy Kimanta,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro  alisema mpaka sasa hakuna fujo wala vurugu zilizotokea.

Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk.Solomon Masangwa amesema mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili ni mafanikio ambayo yanakuja tena kwa miaka inayofuata

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles