27.5 C
Dar es Salaam
Friday, July 1, 2022

Askari wa Marekani atuhumiwa kuua kwa kukusudia

Handout photo of Officer Betty Shelby of the City of Tulsa Police Dept in Tulsa, Oklahoma

Askari Polisi wa Jimbo la Oklahoma, Marekani, Betty Shelby, anatuhumiwa kwa kosa la kufanya mauaji kwa kukusudia dhidi ya mtu asiyekuwa na hatia.

Tukio hilo limeripotiwa na Mwanasheria Mkuu wa Wilaya hiyo Steve Kunzweiler, ambapo alisema mtuhumiwa huyo alimpiga risasi Terence Crutcher (40) baada ya gari yake aina ya SUV kusimama barabarani wiki iliyopita.

“Tumeshapitia madai na ni jukumu letu kufanya maamuzi iwapo kufunguliwa kwa  mashtaka kunatendeka kwa haki chini ya sheria,” alisema Kurnzweiler.

Kurnzweiler aliongeza kuwa kibali cha kukamatwa kwa Shelby kilitolewa na mipango ilifanywa ili aweze kujisalimisha.

Hata hivyo, mlalamikaji dhidi ya askari huyo alisema uwoga ndio ulimfanya Betty aamue haraka  kumpiga risasi Crutcher,  hivyo anatuhumiwa kwa kwenda kiyume cha sheria.

Familia ya Crutcher imefurahishwa na hatua za kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya askari huyo na kuahidi kuwa watapigania haki itendeke.

Kwa upande wake pacha wa kike wa Marehemu Crutcher, Tiffany amesema kuwa huu ni ushindi mdogo na kwamba watahakikisha wanakata cheni ya ukatili unaofanywa na askari polisi kwani wanajua historia nzima.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya Susan Witt, adhabu inayoweza kuchukuliwa kwa kosa la kufanya mauaji ya kukusidia ni kati ya kifungo cha miaka mine au cha maisha.

Naye Gavana Mary Fallin amesema kuwa anaomba mashtaka dhidi ya Shelby yalete amani katika familia ya Crutcher na watu wote wanaoishi Tulsa, lakini pia amewataka watu wawe na subira wakati kesi ikiendelea kufuatiliwa na kwamba askari huyo hana hatia mpaka pale mahakama itakaposema.

Kamera kadhaa ziliweza kurekodi tukio zima la mauaji hayo ambapo Crutcher anaonekana akiwa amenyoosha mikono juu ya kichwa chake na kuelekea kwenye gari lake.

Pamoja na mambo mengine, picha hizo hazikuonyesha kama vioo ama milango ya gari ilikuwa wazi  pia hakukuwa na silaha yoyote ndani ya gari. SOURCE: CNN

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,419FollowersFollow
544,000SubscribersSubscribe

Latest Articles