22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Finca yasamehe mikopo waathirika wa tetemeko

_91164264_5f67b142-82fd-4a1f-a096-d4a5f1e41cc9

Na Mwandishi Wete, KAGERA

BENKI ya Finca Microfinance imewasamehe mikopo yenye thamani ya Sh milioni 57.2 wateja wake 15 waliothibitishwa kuathirika kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu, mkoani Kagera.

Hayo yamesemwa juzi na Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Finca, Aluto Hagamu, wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salim Kijuu, misaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani humo.

Hagamu alisema dhumuni kubwa la benki hiyo la kufuta mikopo hiyo ni kuwapunguzia mzigo wanachama hao kutokana na athari walizozipata kutokana na tetemeko hilo na kuwawezesha kurudi katika shughuli  wanazozifanya ili kujiweka sawa kiuchumi.

“Kwa niaba ya Benki ya Finca, tunatangaza kusamehe mikopo yote yenye thamani ya Sh milioni 57.2 kwa wateja wetu waliokumbwa na tetemeko la ardhi. Pamoja na hali hiyo, pia tunapenda kukabidhi sukari mifuko 25, mabati bando tano pamoja na misumari katoni nane kwa dhumuni la kusaidia waathirika wa tetemeko,” alisema Hagamu.

Akitoa shukrani baada ya kupokea misaada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salim Kijuu, alizitaka taasisi nyingine za fedha kuiga mfano wa benki hiyo wa kusaidia wanachama na waathirika wa tetemeko la ardhi kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles