24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Ariana, Nicki Minaj wakanusha ‘bifu’

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Ariana Grande na Nicki Minaj, wametumia vizuri kurasa zao za Twitter kukanusha taarifa kwamba wawili hao wapo kwenye mgogoro.

Taarifa za mgogoro wa wawili hao zilianza baada ya Nicki Minaj kuachia wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la ‘Bust Down Barbiana’.

Ndani ya wimbo huo kuna maneno ambayo yaliwafanya baadhi ya mashabiki waamini kuwa ni dongo kwa Ariana Grande.

Ariana alikuwa wa kwanza kukanusha taarifa hizo huku akiweka wazi kuwa anaamini Nicki hawezi kufanya kitu kama hicho kwa kuwa hawana mgogoro wowote kati yao.

“Hakuna kitu kibaya kinachoendelea kati yetu, kikubwa ni upendo tu,” alitwiti Ariana.

Hata hivyo Nicki naye alitwiti: “Nakupenda sana Ariana katika maisha yangu yote.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles