24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Chris Brown aomba kupigana na Offset

NEW YORK, MAREKANI

STAA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ameomba pambano dhidi ya rapa kutoka kundi la Migos, Offset, baada ya rapa huyo kumshambulia Chris kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Sababu ya Offset kumshambulia Chris ni baada ya kuposti video ya 21 Savage ambayo inamuonesha akiwa anaimba na msanii kutoka nchini Uingereza ambaye pia ni mchekeshaji, Big Shaq.

Mapema wiki hii, 21 Savage alikamatwa na uhamiaji kwa madai kuwa msanii huyo amezamia nchini Marekani tangu mwaka 2005, wakati yeye ni raia wa nchini Uingereza, hivyo Offset aliona kuwa video ambayo imepostiwa na Chris ilikuwa na udhalilishaji.

Hivyo, Chris amemjia juu Offset huku akimwambia aachane na maisha yake na kama anataka, basi amtafute wakutane ili wamalizane kwa kupigana na si kudhalilishana kwenye mitandao.

“Jaribu kufuatilia maisha yako kama huna mambo ya kufanya, sina mengi ya kuongea lakini kama unataka ni vizuri tukutane na ikiwezekana tupigane ili kiu yako ikatike,” aliandika Chris kwenye ukurasa wake wa Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles