29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Apandishwa kizimbani kwa tuhuma za ulawiti

ERICK MUGISHA Na NEEMA SIGALIYE (TUDARCo) – DAR ES SALAAM

MKAZI wa Sinza jijini Dar es Salaam, Abubakari Bakari (22), amepandishwa kizimbani katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la ulawiti.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Frank Moshi na Mwendesha  Mashtaka wa Serikari,  Yussuf  Aboud, alidai Machi 21 , 2019  eneo la Sinza  wilayani  Kinondoni, Dar es Salaam alimlawiti mtoto wa miaka 12.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo, ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikari, Aboud alisema upelelezi bado ujakamilika.

Hakimu  Moshi  alisema  dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka Serikali za Mtaa na nakala za vitambulisho na kusaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja.

Mshatakiwa huyo alitimiza masharti hayo ya dhamana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba Mosi, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles