29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wanaoishi na VVU wapewa elimu ya fedha

ERICK MUGISHA – DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), limeviwezesha vikundi vya Watu Wanaishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) kupata elimua utunzaji wa fedha.

Mafunzo hayo yalitolewa jana na Shirika lisilo la kiserikali la  JSI, ambapo wamefanikiwa kuwanoa wanachama wa vikundi hivyo kwa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam na Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika mafunzo hayo Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Juma Rajabu alisema kuwa mfumo huo utarahisha utunzaji wa taarifa muhimu hasa zinazohusu masuala ya fedha.

 “Tunakwenda katika mfumo wa kidunia zaidi na napenda kuwashukuru JSI ambao pia ni wadau wakubwa katika kupambana na Ukimwi kwa kuona jitihada hizi na hatimaye kutoa msaada wa programu hii ambayo ni ya kisasa zaidi hii itatusaidi kufikia malengo yetu,” alisema Rajabu

Kwa upande wake Mshauri wa Miradi JSI, Cayus Mrina alisema mfumo huo umetolewa kwa ajili ya urahisishaji wa taarifa kwa watu wanaoishi na VVU ili waweze kujua masuala muhimu katika utunzaji na uandaaji wa taarifa za fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles