24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

‘Angusha’ ya Hennesseyy, Elly Da Bway haikamatiki

Na Christopher Msekena, Mtanzania Digitala

Staa wa Bongo Fleva, Hennesseyy Hennesseyy, ameendeleza ubabe kwenye muziki huo baada ya kufunga wiki hii na mkwaju mpya, Angusha aliomshirikisha Elly Da Bway.

Hennesseyy ambaye ni bosi wa leo ya Spacious Music na Spacious Films, amejizolea umaarufu mkubwa kwa muziki mzuri unaoambatana na video kali zinazolenga kutamba kwa maisha ya kula bata anayoishi.

Akizungumza na mtanzania.co.tz, Hennesseyy ameweka wazi kuwa miongoni mwa ngoma kali alizotumia bajeti kubwa kutoka kwenye albamu yake ni Angusha na tayari mashabiki wameipokea vizuri.

“Maisha ya bata ndio maisha yetu halisi kwahiyo tunachokionyesha kwenye video ndio kile tunachoishi kama Spacious Music, nashukuru mapokea ya Angusha yamekuwa mazuri kwasababu tumeendelea kukaza kwa kutoa video za gharama na muziki mzuri kama kawaida yetu,” amesema Hennesseyy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles