25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Amunike ; hatujatoka kapa kwa Misri

NA MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

LICHA ya kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike amesema ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake, katika mchezo huo.

Stars ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wa fainali za Mataifa Afrika (Afcon), Misri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Borg El Arab, Alexandria.

Mchezo huo ulikuwa wa kujipima nguvu, kwa ajili ya kujiandaa na fainali hizo zitakazoanza kutimua vumbi Juni 21, mwaka huu.

Katika michuano hiyo, Stars imepangwa kundi C, pamoja na timu za Algeria, Senegal na majirani zao, Kenya.

Stars itazindua kampeni zake kwa kuvaana na Senegal, Juni 23, kisha kuchuana na Kenya juni 27, kabla ya kumaliza hatua ya makundi kwa kuivaa Algeria, Juni 30.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Amunike, alisema wamekutana na moja ya timu bora ya Taifa katika nchi za Afrika na imekuwa kipimo kizuri kwao.

“Mchezo ulikuwa mzuri, timu yangu ilicheza vizuri pia, tulipata nafasi chache tukashindwa kuzitumia, hata hivyo ukweli vijana wangu walicheza kwa kufuata maelekezo niliyowapa na kutimiza majukumu yao, tunakwenda kusahihisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo huo, ili yasitokee kwenye mechi zetu zijazo,” alisema kocha huyo raia wa Nigeria.

Kwa upande wake, nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta alisema ugumu waliokutana nao katika mchezo huo, utawasadia kujenga hali ya kujiamini kuelekea katika hatua ya makundi.

“Misri wana timu nzuri, wachezaji wao wako fiti, lakini unapocheza mechi ya kirafiki ngumu unajua makosa yako na kufahamu sehemu gani unatakiwa kurekebisha kabla ya kuingia katika mashindano.

“Hatua ya makundi haitakuwa rahisi, ugumu   tuliokutana nao kwa Misri, ndio itakavyokuwa katika mechi ya hatua  ya  makundi, nafikiri walimu wameona  makosa na watayafanyia kazi,” alisema Samatta

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles