27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

AMBER LULU: NARINGIA MAJALIWA, SIYO MCHINA!

AMBER LULU
AMBER LULU

NA KYALAA SEHEYE,

MUZIKI wa Bongo Fleva unaendelea kupaa siku hadi siku, huku video za nyimbo zao zikiwa kichochoe cha kupaa kwa wasanii husika.

Hata hivyo kati ya vitu vinavyozidisha ladha katika video hizo ni mamodo wanaocheza katika kazi za wasanii hao wanaojulikana kama video queen a.k.a video vixen.

Hapo sasa ndipo unapokutana na jina la Amber Lulu. Ukweli ni kwamba ukizungumzia mamodo  wanaobamba mbaya Bongo, lazima umtaje mrembo huyu mwenye figa inayowatoa udenda wanaume wanaopenda ‘vitu vizuri’.

Anaitwa Lulu Mkongwa ‘Amber Lulu’, ambaye nje ya kazi yake hiyo, anasumbua sana kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kutokana na picha zake matata zenye mapozi ya nguvu.

Umaarufu wa Amber Lulu ulipaa zaidi pale picha zake za utupu ziliposambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ambazo inaelezwa kuwa, aliyefanya hivyo ni aliyekuwa  mpenzi wake.

Jina la mpenzi wake huyo halijatajwa popote, lakini wafuatiliaji wa mambo ya burudani wanamtaja kuwa ni msanii anayechipukia katika Bongo Fleva, mwenye asili ya Asia.

Polisi wa Swaggaz alifanya naye mahojiano na kuzungumza mengi ikiwemo skendo hiyo.

Akizungumzia hilo, Amber Lulu anasema: “Ni skendo iliyoniumiza sana kwa kweli na naweza kusema mpaka sasa bado inaniumiza, ila nashukuru Mungu angalau sasa nimeanza kusahau.”

MY STYLE: Unaweza kueleza, wewe una tofauti gani na mamodo wengine?

AMBER LULU: Mimi ni mtulivu, mchangamfu, pia huwa nipo kikazi zaidi. Nipo makini na kazi na ninajua ninachofanya, kifupi ni mtu wa mipango. Sikurupuki kwenye mambo yangu. Hiyo ndiyo tofauti yangu kubwa na mamodo wengine.

MY STYLE: Kitu gani unajivunia katika kazi yako ya umodo?

AMBER LULU: Kwa kweli kazi hii imenifanya nikutane na watu wengi wenye kujielewa na kujua thamani ya mtu, pia nashukuru kupitia hii kazi, nimeweza kujijua na kujielewa.

MY STYLE: Unapenda mwanaume mwenye sifa zipi?

AMBER LULU: Napenda mtu anayejituma katika kutafuta, mwelewa na mwenye upendo wa kweli kwangu na familia yetu tutakayojaliwa.

MY STYLE: Unawazungumziaje mamodo wanaokuja kwenye fani hii na kutumia mkorogo ili waonekane warembo?

AMBER LULU: Nawashauri wapende ngozi zao, kwani kuwa modo siyo weupe, ni mwonekano pia ngozi asili ndiyo inayotakiwa…  inabidi kutumia akili ya ziada katika kutumia vipodozi, utafanikiwa miaka miwili mitatu baada ya hapo, unapoteza mwelekeo kwa kuwa ngozi inaharibika.

MY STYLE: Unazungumziaje shepu yako ambayo kwa sasa imekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii wengi wakidai ni Mchina?

AMBER LULU: Hii ni shepu yangu halisi na ninamshukuru Mungu kwa uumbaji na pia wazazi wangu, mimi niko kihalisia zaidi, sijaongeza chochote na wala sivai chochote ni majaaliwa ya Mungu.

MY STYLE: Ulijisikiaje mpenzi wako alipovujisha picha  zako ulizopiga faragha?

AMBER LULU: Kwa kweli iliniumiza sana, ile siku tulitoka club na tulikuwa tumelewa, sipendi kuliongelea sana hili jambo linaniumiza japo limeshapita.

Lakini mimi nawashauri wasichana wenzangu, tuache kabisa tabia ya kupiga picha za faragha. Unaweza kufanya hivyo kwa mapenzi tu, lakini baadaye inaweza kuwa athari kubwa kama ilivyotokea kwangu.

Kwakweli wasichana tuwe makini sana kwa hilo. Wanaume wana maneno matamu sana na wakitaka lolote, watatumia maneno yoyote mpaka watahakikisha wamepata walichotaka, lakini mwisho wake ndiyo huo tena kama ilivyokuwa kwangu.

MY STYLE: Katika madini yaliyopo Tanzania, unapenda zaidi madini ya aina gani?

AMBER LULU: Mimi napenda sana Tanzanite, yale madini yanayopatikana kule Mirerani, Manyara. Ningekuwa na fedha, kila ninachovaa kingekuwa kimenakshiwa na Tanzanite.

MY STYLE: Gari gani ndiyo la ndoto zako? Yaani ukiwa ndani ya ndinga gani, utajisikia raha na amani zaidi?

AMBER LULU: Mh! Kwa kweli nikiwa na gari aina ya AUDI A8 toleo jipya la mwaka huu, roho yangu itakuwa kwatu.

MY STYLE: Asante Amber Lulu kwa muda wako.

AMBER LULU: Nashukuru pia, karibu tena dada.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles