26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

ALLY KIBA AWACHANA MASTAA WA KIKE

NA SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM


NYOTA wa Bongo Fleva Afrika Mashariki na Kati, Ally Kiba, amewataka wanawake maarufu kwenye soko la muziki na filamu Tanzania, kuitumia ipasavyo mitandao ya kijamii kwa manufaa ya maisha yao ya sasa na baadaye.

Kiba, anayetamba na ngoma ya ‘Mvumo wa Radi’, aliyasema hayo juzi alipohojiwa na kituo kimoja cha runinga jijini Dar es Salaam.

Katika mahojiano na mwandishi wa runinga hiyo, Ally Kiba, aliwatolea povu mastaa wa Bongo akiwataka waache  maisha ya kuigiza na kujianika uchi mitandaoni.

“Stara ni kitu kizuri sana katika jamii na maisha yetu kwa ujumla, mastaa wengi hasa dada zetu wanaamini kukaa utupu ndio kupendwa, lakini sisi wanaume hatuko hivyo,” alisema Kiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles