24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Akamatwa nyumba ya wageni na mwanafunzi darasa la saba

Malima Lubasha – Musoma

JESHI la Polisi mkoani Mara,linamshikilia mwendesha pikipiki maarufu bodaboda mkazi wa Mtaa wa Morembe mjini Musoma kwa kutuhuma za kumrubuni mwanafunzi  wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 13 na kwenda naye nyumba ya kulala wageni nyakati za usiku.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,Daniel Shilla alithibitisha kuwapo tukio hilo.

Alimtaja mtuhumiwa kuwa ni, Kelvin Andrea(17) na kusema tuko hilo lilitokea Aprili 16, mwaka huu saa 6.30 usiku.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa akiwa na binti huyo mdogo mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Bweri.

Alisema alikamatwa wakiwa nyumba ya kulala ya Lipando na kufafanua upelelezi  utakapokamilika  atafikishwa mahakamani.

Alisema mwanafunzi yupo nyumbani kipindi hiki  ambacho shule zimefungwa kutokana na ugonjwa wa corona ili kujiepusha na msongamano.

Kutokana na hali hiyo, Kamanda Shilla alitoa wito kwa wazazi  walezi kuwalinda watoto wao, badala ya kuwaacha wakizurura na kukutwa nyumba za wageni.

Imeelezwa vitendo vya kubaka,kulawiti na ukatili wa kijinsia hususani watoto wenye umri chini ya miaka 18, vimekuwa  vikiripotiwa vituo mbalimbali vya polisi mkoani hapa kila mara, lakini jamii  inashindwa kutoa ushirikiano.  

Mwenyekiti wa Mtaa wa Morembe Kati,Juma Maka alisema alipokea taarifa za tukio na kuamua kulifuatilia hadi kufanikiwa kumkamata mhusika.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles