30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Mabasi yanayojaza abiria kufutiwa leseni

Murugwa Thomas, Tabora

KATIKA kuhakikisha Mkoa wa Tabora, unakabiliana na maambukizi  ugonjwa wa corona,umesema utayafutia leseni magari yanayaojaza abiria kupita kiasi.

Agizo hilo, limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Agrrey Mwanri alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Mwanri aliwaagiza wakuu wa wilaya kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha magari yatakayokiuka agizo hilo, wamiliki wake wanyang’anywe leseni.

Alisema kuna malalamiko yaliyotolewa na abiria kuwa baadhi ya madereva na makondakta wa magari yanayotoa huduma ya usafiri kutoka wilaya na mkoa huo,hulazimisha kujaza abiria hadi wanasimama ndipo wanaondoa gari kituoni.

Alisema kitendo hicho kinapingana na maagizo na maelekezo yanayotolewa na viongozi na wataalamu wa afya juu ya kujikinga na maambukizi ya corona.

Pia aliwaagiza watendaji kushirikiana na jeshi la polisi kuwakamata wale wote watakaokutwa wakiuza bei kubwa vifaa vinavyotumika kukabiliana na ugonjwa huo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles