25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ajira zilizotolewa kwa miaka mitatu zatajwa

ANDREW MSECHU

KATIBU wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi amesema Watanzania 587,746 kati ya 594,300 walioomba ajira kufikiaDesemba 15, mwaka huu wamekosa ajira serikalini.

Idadi hiyo ni sawa na asilimia 98.89 kati ya watu walioombaajira serikalini tangu Novemba 2015, ikiwa ni miaka mitatu tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano.

Akizungumzia utekelezaji wa Sekretarieti ya Ajira katika   miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Daudi alisema kati ya walioomba ajira hizo ni watu 140,000 pekee walioitwa kwenye usaili kwa ajili ya kujaza nafasi 6,554 zilizotangazwa kuwa wazi.

“Tangu Serikali iingie madarakani Sekretarieti ya Ajira imetangaza nafasi za kazi 6,554 kwa ajili ya wizara, idara, wakala,sekretarieti za mikoa, manispaa, halmashauri na taasisi mbalimbali za elimu.

“Hadi kufikia Desemba 15, 2018   nafasi wazi za kazi 6,099 zilishajazwa na nafasi 455 zilizotangazwa kati ya  Novemba na Desemba 2018 mchakato wake unaendeleana unatarajiwa kukamilika hivi karibuni,” alisema.

Alisema idadi hiyo ya watumishi serikalini ni ilei nayoshughulikiwa moja kwa moja na sekretarieti anayoiongoza  ila kuna ajira nyingine za watumishi wanaoajiriwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa (TAMISEMI) katika kada za afya na elimu ambazo sekretarieti pia hushiriki katika usimamizi.

Alisema katika ajira hizo za TAMISEMI  kwa kipindi hicho cha miaka mitatu watumishi 24,728 wa kada ya afya wameajiriwa na watumishi 40,086 wa kada za walimu wameajiriwa, hivyo kufikisha watumishi 64,814 walioajiriwa katika kada za afya na walimu.

“Hata hivyo, idadi hii inaweza kuongezeka katika mwaka wa fedha wa 2018/19 kwa watumishi watakaoajiriwa kwa kada za walimu, afya  na watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo utaratibu wake wa ajira unaratibiwa na mamlaka husika,” alisema.

Daudi alisema Sekretarieti ya Ajira imesema imeboresha huduma zake kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa kuanzisha mfumo wa elektroniki wa utumaji maombi ya kazi ujulikanao kama ‘recruitmentportal’.

Alisema kupitia mfumo huo unaopatikana kwa anuani yaportal.ajira.go.tz ulioanza mwaka 2014/15 ambako tayari zaidi ya watu 300,500 wamekwisha kujiandikisha na maombi 594,200 ya kazi yamekwisha kuwasilishwakupitia mfumo huo.

Alisema   mfumo huo umekuwa wa mafanikio kwa kusaidia kupunguza mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi siku 52, kupunguza malalamiko ya waombaji kuhusu upotevu wa barua zao za maombi na kupunguza ufinyu wa nafasi za kutunza nyaraka za maombi ya kazi.

Alisema kati ya mwaka 2015 hadi 2018 nakala za vyeti vyawaombaji 18,817 viliwasilishwa kwenye mamlaka zinazohusika na utoaji wa vyeti hivyo kwa ajili ya uhakiki na katika vyeti hivyo, halali vilikuwa 18,112 na vyeti 706 vilibainika kuwa vya kughushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles