23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali za barabarani zapukutisha watu

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

TAKWIMU za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha watu milioni 1.35 hufariki kila mwaka duniani kutokana na ajali za barabarani huku katika Bara la Afrika zikionyesha katika kila watu 100,000, wanaofariki ni 24.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mkoa wa Dodoma, Marry Munissi, alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga wa ajali za barabarani nchini.

Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwa kushirikiana na TLS Mkoa wa Dodoma.

Munissi alisema ajali za barabarani zimekuwa zikigharimu maisha ya watu, hususani katika nchi za Afrika.

Alisema Bara la Afrika linaongoza kwa kuwa na ajali nyingi za barabarani duniani licha ya kuwa lina magari kwa asilimia 2.

Munisi alisema takwimu zinaonyesha watu millioni 1.35 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, hivyo hawana budi kupinga na kuzuia kwani inaathiliri uchumi wa nchi.

“Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kimeandaa kumbukumbu hii ili kupinga ajali za barabrani, ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuzuia athari za ajali hizo,” alisema Munissi.

Alitoa wito kwa Serikali ili kupunguza ajali za barabarani ifanye marekebisho ya sheria ya usalama barabarani ya 1973 katika kiwango cha ulevi anachotakiwa kuwa nacho dereva na masharti ya mwendokasi.

Alisema anaamini Bunge lijalo linaweza kufanya marekebisho ya sheria kwani walishapeleka mapendekezo serikalini.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, SP Prackson Rugazila alisema kwa upande wa Tanzania vidhibiti mwendo vimesaidia sana kupunguza ajali za barabarani.

“Hivi sasa ajali za barabarani hapa Tanzania zimepungua sana na hii ni kutokana na vidhibiti mwendo ambavyo vimefungwa katika mabasi ya abiria na baadhi ya magari,” alisema SP Rugazila.

Mwathirika wa ajali za barabarani, Dismas Mnyeke alisema amepoteza mguu mmoja kutokana na uzembe wa dereva wa basi alilokuwa amelipanda ambaye alikuwa akikimbizana na gari lingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles