24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Ajali ya basi yaua wanne Iringa

Na Mwandishi Wetu, Iringa

WATU wanne wamefariki dunia katika ajali ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Luwinzo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Ajali hiyo ilitokea jana wilayani hapa kwa kuhusisha basi hilo lenye namba za usajili T 782 ACR linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es salaam ambalo lilipata ajali asubuhi katika eneo la Kinegembasi Kata ya Mbalamaziwa.

Basi hilo lililokuwa likisafiri kutokea Njombe kuelekea Dar es Salaam liligongana na lori lenye namba za usajilli T 718 CRV aina ya IVECO ambalo lilikuwa nalo lilikuwa likitokea mkoani Ruma.

Kamanda  wa Polisi Mkoa  wa Iringa, Kamishana Msaidizi wa Polisi, Peter Kakamba, alisema ajali  imeua watu wanane na kujeruhi zaidi ya watu 30 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya Mufindi.

Kamanda Kakamba  alisema  katika ajali  hiyo watu  wanne walifaridi dunia wakiwemo wahudumu wa basi hilo, waliotambuliwa kwa majina ya Rashid Kibarabara ( 47) , Salim Chengula (28), ambao walifariki dunia papo hapo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, amethibitisha kupokea miili ya watu wanne waliopoteza maisha na wengine 32 waliojeruhiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles