24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Airtel, Letshego wazindua Vimba na Timiza na Ushinde

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money Timiza Akiba kwa ushirikiano na Benki ya Letshego Tanzania wamezindua promosheni ya kuweka akiba kidigitali ‘Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo wateja wa Airtel Money watapata nafasi ya kujishindia bajaji, pikipiki luninga ya flati na pesa taslimu kila wanaweka akiba kupitia Airtel Money Timiza akiba Airtel Money Timiza Akiba ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Money kuweka akiba kidigital wakiwa popote.

Akizungumza Dar es Salaam Machi 28, 2023 wakati akitangaza kuzindua promosheni hiyo mpya, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando amesema, ‘Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde inalenga kuhuisha na kuhamasisha wateja wa Airtel Money na jamii kwa ujumla kujijenga utamaduni wa kuweka akiba kidigitali.

“Airtel Money tunajisikia fahari sana tunapoendeleza ubunifu katika huduma hii ya Airtel Money inayokuwa kwa kasi huku wateja wakijihudumia kidigitali kupitia Airtel Money, amesema Singano na kuongeza kuwa Airtel Tanzania imeshirikiana na Benki ya Letshego Tanzania kuendesha promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili (wiki 8) kuanzia leo.

“Promosheni ya Airtel Money Vimba na Timiza Akiba Ushinde itawazadia wateja wote wa Airtel Money wanaoweka akiba kupitia Timiza akiba kuanzia wiki hii ambapo hadi kufikia mwisho wa promoshen wateja 203 watakuwa wameibuka washindi wa promosheni hii.

“Tutakuwa na droo moja kila wiki ambapo Wateja 25 watashijishindia Sh 20,000 kila mmoja na tutawawekewa pesa zao za zawadi moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money, vilevile tutatoa zawadi ya bajaji mpya, pikipipiki mpya, pamoja na luninga mpya (flatscreen) kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii,” amesema Mmbando.

Nae Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko wa Benki ya Letshego Tanzania, Leah Phil amesema: “Benki ya Letshego Tanzania tunajivunia ushrikiano wetu na Airtel Money kupitia huduma hii ya kujiwekezea kidigitali, tunawahakikishia wateja wote wa Airtel Money wenaotumia Timiza Akiba kwamba watapata zawadi zao za ushindi kwenye akaunti zao za Airtel Money zao mara tu watakapotangazwa kuwa washindi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,207FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles