26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CRS yaadhimisha miaka 60, yaahidi kuendelea kusaidia wenye uhitaji

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Shirika la Catholic Relief Services (CRS) limeazimisha miaka 60 tangu kuwepo kwake hapa nchini waka wa 60 wa kuwepo nchini Tanzania na kuahidi kuendelea kuwasaidia watu wanaoshi katika mazingira magumu hususan maeneo ya vijijini.

Maadhiminisho hayo yamefanyika Machi 28, 2023 jijini Dar es Salaam ikihusisha viongozi mbalimbali wa shirika hilo, wahisani, wafanyakazi na viongozi wa kitaifa.

Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Catholic Relief Services, Sean Callahan.

Akizungumza katika tukio hilo Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Catholic Relief Services, Sean Callahan amesema ni heshima kwao kuwapo nchini kwa kipindi chote ikifanya kazi bega kwa bega na kanisa katoliki.

“Wakati CRS duniani inatimiza miaka 80, ni heshima kubwa kuwapo Tanzania kwa miaka 60, tukifanya kazi bega kwa bega na Kanisa Katoliki, washirika wetu wa maendeleo na jumuiya tunazohudumia, na kazi hii inaendelea kuwa jukumu kubwa kwetu kutokana na uaminifu tuliopewa,” amesema Callahan.

Aidha, CRS imekuwa ikihudumia jumuiya za Kitanzania tangu 1962, kipindi ambacho mahitaji ya kibinadamu yamefikia kiwango cha juu zaidi duniani.

“Tunaendelea kuunga mkono mabadiliko yanayochochewa na jamii kwa kiwango kikubwa nchini kwa kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa dini mbalimbali, washirika wa kitaifa na jamii mbalimbali katika njia yao ya ustawi na ustahimilivu dhidi ya athari mbaya za changamoto kuu za leo.

“Ikiwa ni pamoja na masuala ya jinsia, upatikanaji wa masoko na fedha kwa vijana, uhaba wa chakula na mabadiliko, ikiwa ni pamoja na ukuta wa kumbukumbu unaoonyesha mafanikio makubwa ya CRS kwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania, maonyesho ya programu za sasa na zilizopita.

“Catholic Relief Services (CRS) imekuwa ikifanya kazi na watu wanaoishi katika mazingira magumu zaidi katika jamii za vijijini nchini Tanzania tangu mwaka 1962. leo programu ya nchi hii inasaidia miradi ya afya, lishe na maendeleo ya utotoni, ushirikishwaji wa kijinsia, uwezeshaji vijana na ujasiriamali, mabadiliko ya tabianchi, maji na usafi wa mazingira(WASH),” amesema Callahan.

Ameongeza kuwa kazi ya misaada na maendeleo ya CRS inakamilishwa kupitia programu za kukabiliana na dharura, VVU, afya, kilimo, elimu, fedha na kujenga amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles