24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Afrika yataka viti vya kudumu UN

UN, NEW YORK


RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesema ipo haja kwa bara la Afrika kuwa na nafasi za kudumu kwenye vyombo vikuu vya maamuzi vya Umoja wa Mataifa

Akizungumza pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA), Kenyatta alisema mwito huo ni kwa vile bara hili linastahili.

“Kenya inaungana na mataifa mengine kutaka Afrika ipewe viti viwili vya kudumu vyenye haki na majukumu sawa na wengine ikiwemo haki ya kura ya turufu, pamoja na viti vingine zaidi, ambavyo si vya kudumu.

“Afrika haijawakilishwa vya kutosha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na hatujawakilishwa kabisa katika kiwango cha kudumu. Ukosefu huu wa haki wa kihistoria ni ishara ya wazi ya mfumo wenye upendeleo unaochangia upungufu wa kutoaminiana kati ya mataifa.”

Naye nyota wa zamani wa kimataifa wa soka, Rais wa Liberia, George Weah, alihutubia kikao hicho kwa mara ya kwanza na kusema matatizo ya uongozi ni mengi.

Weah alikiambia kikao hicho kuwa Liberia itaanza misururu ya mazungumzo ya amani, ili wasirudie makosa ya kale yaliyowasababishia hasara.

Hali ilikuwa tofauti mwaka huu kuhusu hotuba ya Rais wa Zimbabwe, tofauti na Rais wa zamani, Robert Mugabe, aliyekuwa mshambulizi mkali dhidi ya nchi za Magharibi, Rais mpya Emmerson Mnangagwa alionekana kutaka kuwa mwanachama anayewajibika katika Umoja huo.

Huku akitaka kuvutia wawekezaji ili kuinua uchumi ambao umeporomoka, Mnangagwa alitoa wito wa kutaka vikwazo ambavyo alivitaja kuwa vimeendelea kuwepo kinyume na sheria, kuondolewa bila masharti:

Mnangagwa alisisitiza haja ya amani, umoja na kuvumiliana huku akisisitiza kuwa nchi yake imefungua milango kwa biashara.

Kikao hicho kimeingia siku yake ya tatu jana, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Augustine Mahiga alihutubia kikao hicho kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli ambaye hakuhudhuria

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles