27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ABU mbinu mpya ya kuandaa vijana  wabobevu katika sekta ya madini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), mdau mashuhuri katika tasnia ya madini nchini Tanzania kwa zaidi ya miongo miwili, imekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia suala muhimu la uhaba wa ujuzi na ukuzaji vipaji ndani ya sekta hiyo. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, GGML haijazingatia tu ubora wa utendaji kazi bali pia kuwekeza katika nguvu kazi ya baadaye ya Tanzania.

Kwa kutambua umuhimu wa kuandaa wafanyakazi wa baadaye na kukuza vipaji, GGML, kwa kushirikiana na wadau wengine, ilitoa mchango mkubwa wa zaidi ya dola milioni mbili mwaka 2009 katika kuandaa mitaala kuandaa vijana wa Kitanzania kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Moshi. Mpango huu umezaa matunda kwa miaka mingi, ambapo zaidi ya vijana 1,400 wamepata mafunzo ya uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi, hivyo kusaidia kupunguza uhaba wa ujuzi katika sekta hiyo.

 Wahitimu 40 wa vyuo mbalimbali nchini ambao wanatarajia kuanza mpango wa mafunzo kazini kwa vitendo unaodhaminiwa na kampuni ya GGML kwa mwaka 2024/2025 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukaribishwa rasmi mwishoni mwa wiki mkoani Geita.

Hata hivyo, dhamira ya GGML katika kukuza vipaji inazidi mafunzo ya ufundi stadi. Mnamo 2009, kampuni ilizindua mpango wa kuajiri wahitimu ili kutoa fursa za mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa vyuo vikuu wasio na ajira. Programu hiyo ilikuwa na idadi ya wahitimu 12 kila mwaka hadi mwaka 2012. Baada ya kusitishwa kwa miaka mitano, GGML ya 2017 ilirjesha programu ya mafunzo kwa vitendo, ikiwapa vijana wa Kitanzania uzoefu muhimu wa kufanya kazi ndani ya GGML kwa mwaka, huku ikiwaruhusu kubobea zaidi katika fani zao. Kati ya 2017 na 2023, GGML ilichukua wahitimu 194 kwenye programu yake ya mafunzo tarajali.

Katika kupanua mafunzo hayo, mwaka huu 2024, kampuni hiyo imekuja na programu iliyopewa jina la African Business Unit (ABU) ambayo  ni zaidi ya program ya mafunzo Taraji ynayaotolewa kwa mwaka. Katika progamu hiyo ya ABU, jumla ya wahitimu 10 wa mafunzo tarajali kwa mwaka jana wamechaguliwa kuendelea na program hiyo ambayo mbali na kupata mafunzo ya juu zaidi pia wamepata ajira za kudumu ndani ya GGML.

Menejea Mwandamizi wa masuala ya Rasilimali watu, Charles Masubi anasema dhumuni la kuwa na mafunzo hayo tarajali kwa wahitimu wa vyuo vikuu kwanza ni kushirikiana na serikali kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi stahiki.

“Lakini pili, kwetu sisi GGML ina maana kubwa zaidi ya hapo kwani tunaandaa wafanyakazi wetu wa baadae tunatengeneza vipaji ambavyo huwa tunavichukua baada ya kuvinoa kutoka kwa wahitimu na kuwaajiri.

Meneja Mwandamizi wa masuala ya Rasilimali watu kutoka GGML, Charles Masubi (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella (kushoto) wakati wa uzinduzi wa programu ya mafunzo tarajali ya GGML kwa 2024/2025. Katikati yao ni Makamu wa Rais Mwandamizi wa AngloGold Ashanti – Kitengo cha Ubia na Ushirika Afrika kutoka AngloGold Ashant – GGML, Terry Strong na Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi Tanzania, Eng.Benjamin Mchwampaka.

“Mbali na kuwafundisha kwa mwaka mmoja, pia tunawapatia kila maarifa wanayohitaji kwenye eneo lao la utaalam kama ni mhandisi tunahakikisha tunamfundisha na kumpa maarifa yote kwa vitendo akisimamiwa na wahandisi wabobevu,” anasema.

Masubi anasema program hiyo ya ABU inawajumuisha wahitimu wa vyuo mbalimbali waliomaliza progamu ya mafunzo tarajali kwa mwaka mmoja ndani ya GGML.

Hii ina maana kuwa baada ya kumaliza mafunzo hayo tarajali wahitimu waliofanya vizuri wanaunganishwa na waliopo kwenye migodi mingine ya Afrika ambapo wanafanya program kama hiyo ya GGML.

“Kisha tunawapa mafunzo ya juu zaidi ya ujuzi au juu ya elimu yao ya darasani, kama ni mhandisi tutamfundisha kuweka vipaumbele, makubaliano, kuandaa bajeti kupata ujuzi wa namna ya kuwasiliana kwa usahihi na wenzake. Kwa sababu vyote hivyo ni muhimu katika kufanya kazi,” anasema Masubi.

Anasema waashiriki wa program hiyo ya ABU, watashirikiana na migodi ya Afrika iliyo chini ya kampuni mama ya AngloGold Ashanti kwenye nchi za Ghana, Guinea.

“Wote watakuwa kwenye program inayofanana na lakini bado wakiendelea kubobea zaidi kwenye fani zao na kufanya mzunguko wa kujifunza zaidi kwenye migodi mingine.

“Hawa watu hatuwaandai kuishia kuwa wafanyakazi wa ngazi za chini, wakati mwingine tunawaandalia fursa ya kupanda juu na kuwa viongozi wakubwa wa kampuni haopo baadae,’ anasema Masubi na kuongeza;

“Tunapokuwa na programu ya pamoja tunatengeneza kiongozi ambaye atafahamu mila na desturi zetu za kazi kama kampuni, utamaduni wetu wa kazi, miiko yetu kila kitu kuhusu kampuni kwa hiyo ikitokea kiongozi huyu amepata nafasi kufanya kazi Ghana atakuwa na ufahamu wa kutosha.

“Atakwenda akiwa ameiva kwenye nyanja zote tunazozingatia AngloGold Ashanti mfano masuala ya uhasibu, uhandisi, mawasiliano, lazima awe vizuri kwa hiyo anakuwa mtaalam ambaye anaweza kuwa kwenye idara yoyote na kufanya kazi vizuri na kukua. Hilo ndio lengo kubwa la  kuanzishwa kwa ABU,’ anasema Masubi.

Mmoja wa wahitimu hao ni Diana Laswai ambaye mbali na kuishukuru GGML pia waliishukuru Serikali kwa kuendelea kuhamasisha sekta binafsi kutoa mafunzo kazini kwa vitendo.

Pia alitoa wito kwa wanafunzi wapya wanaoanza mafunzo hayo mwaka huu  kufanya kazi kwa bidii, kuzingatia nidhamu na kuzingatia tunu za GGML ambavyo ni usalama.

Evelyne Julius ambaye ni mhandisi wa masuala ya umeme naye anasema “nimejifunza vitu vingi. Uwepo wangu GGML ni fursa ya kipekee kwa sababu nitaweza kutekeleza miradi mbalimbali kwa ujasiri na ujuzi nilioupata,” alisema.

Mkunde Frank ambaye ni mteknolojia wa masuala ya jiolojia, naye anasema nafasi aliyoipata ya kuendelea kufanya kazi ndani ya GGML kupitia progamu ya ABU, imeendelea kumjengea kujiamini na kunoa zaidi ujuzi wake.

“Mathalani kwenye kitengo cha geolojia tumepata fursa ya kipekee, kila mfanyakazi anapewa uthamani bila kujali mkubwa au mdogo. Lakini hata ukishuka kwenye machimbo chini ya ardhi kila mfanyakazi anazingatia mafunzo aliyopewa kwa vitendo hasa katika kutekeleza kipaumbele cha kwanza ambacho ni usalama,” anasema.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Ujuzi, Albert Rukeisa (kushoto) akizungumza na Meneja Mwandamizi wa masuala ya Rasilimali watu kutoka GGML, Charles Masubi (kulia) katika hafla ya kuwakaribisha wahitimu 40 wa vyuo mbalimbali wasio na ajira ambao wamepatiwa fursa ndani ya GGML kupata mafunzo ya vitendo kazini kwa muda wa mwaka mmoja sambamba na wahitimu 10 wa mafunzo huo kwa mwaka jana ambao wamepata ajira ya kudumu ndani ya kampuni hiyo.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Ujuzi kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Albert Rukeisa anasema hitihada hizo za GGML kwa zaidi ya miaka 15 zimekuwa chachu kwa waajiri wengine kuendelea kutoa nafasi kwa vijana kujifunza na kuongeza wataalam wa madini katika sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles