25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Abdul Nondo arejeshwa chuoni UDSM

Asha Bani, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo, amerejeshwa chuoni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alikokuwa akisoma.

Nondo amepokea barua ya kurejeshwa chuoni hapo leo Ijumaa Januari 4, baada ya kusimamishwa masomo mwaka jana kutokana na kesi ya kudanganya kutekwa na kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni iliyokuwa ikimkabili, ambapo kwa mujibu wa sheria za chuo hicho uongozi ulilazimika kumsimamisha masomo hadi atakapomaliza kesi hiyo.

“Barua hii imethibitisha mimi kurudishiwa sifa ya kuwa mwanafunzi wa UDSM kuanzia tarehe 6/1/2019 ambapo nitakuwa na haki ya kufanya maandalizi na kufuatilia taratibu zote za kujiandaa kuendelea na masomo semista ya pili kuanzia Machi 2019.

“Ikumbukwe mimi nilibakiza semista ya pili tu ya mwaka wa tatu ndiyo naanza kufuatilia taratibu za kumalizia semista hiyo hapo mwezi wa tatu baada ya mimi kupata barua hii ya kurejeshewa sifa yangu (status) ya uanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam. ni muda wa kujipanga kumalizia masomo yangu, hili ni jambo la msingi sana,” amesema Nondo katika taarifa yake.

Nondo alishinda kesi hiyo na kuachiwa huru Novemba 5, mwaka jana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa kushindwa kumtia hatiani na upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha makosa aliyoshtakiwa nayo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles