33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mgombea udiwani Jangwani aiomba NEC kumrejesha kwenye kinyang’anyiro

BRIGHITA MASAKI-DAR ES SALAAM

Wakati Wagombea wa nafasi mbalimbali wakiendelea na kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mgombea udiwani Kata ya Jangwani (Chadema), Furaha Ambikile ameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumrejesha kwenye kinyang’anyilo hicho ili akahukumiwe na wananchi.

Ambikile ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 21, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesisitiza kuwa ni jambo linaloshangaza kuona hadi sasa jina lake bado halijarudi ikilinganishwa kuwa siku za kampeni zinazidi kupukutika.

“Agosti 12, mwaka huu nilienda kuchukua fomu kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi Kata ya jangwani lakini kwa bahati mbaya baada ya kuchukua fomu hiyo na kuijaza chini ya wanasheria wa chama, Agosti 25 nilirejesha fomu kisha siku hiyo nikawa nimeteuliwa kuwa mgombea udiwani kata ya Jangwani.

“Lakini Agosti 28, nilipewa taarifa ya kuenguliwa kuendelea na mchakato kwa madai ya kuwekwa pingamizi na wagombea wa vyama vya CCM na CUF, baada ya hapo tukajibu hoja moja baada ya nyingine, baadaye NEC ikaweka wazi kuwa imepokea rufaa zote na inaanza kuzifanyia kazi.

“Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba licha ya NEC kutoa majibu ya rufaa zingine bado rufaa yangu haijatolewa majibu kwa madai kuwa bado haijajadiliwa jambo ambalo nimechoka, ni bora NEC ikanirejesha ili nikakataliwe na wananchi wenyewe, kwani inaonekane kwamba sifanyi mikutano kwa wananchi wangu jambo ambalo siyo kweli, ” amesema Ambikile.

Ambikile ameongeza kuwa ni jambo linalosikitisha kuona kwamba hadi leo siku ya 36 hajapata barua ambapo amelalamika kuwa jambo hilo ni kinyume na katiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles