30.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane aanza mikakati ya kumnasa Mbappe

 MADRID,HISPANIA 

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane ataingia sokoni kusaka mshambuliaji katika dirisha hili la usajili ili kukiongezea nguvu kikosi chake kinachokabiliwa na kazi ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Hispania msimu ujao. 

Baada ya kutolewa na Manchester City katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mbingwa Ulaya, Zidane ana kazi moja ya kuhakikisha anatetea ubingwa huo dhidi ya wapinzani wao, Barcelona. 

Zidane amemtaja Kylian Mbappe kama chaguo lake namba moja katika usajili huo, akilenga kumuunganisha na Karim Benzema katika idara ya ushambuliaji. 

Kikosi cha Zidane si kipana kikiwa na vijana wachanga Marco Asensio, Lucas Vasquez, Luka Jovic na Federico Valverde ambao nao hawakuwa na uwezo wa kuisadia Madrid mbele ya City Ijumaa iliyopita. 

Gareth Bale alikuwa chaguo la Zidane, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Wales anaripotiwa kuwa alimwambia Zidane hataki kusafiri na timu hiyo kwenda Manchester kwa ajili ya mchezo huo.

Mbappe amekuwa ni mchezaji anayependekezwa na Zidane baad ya Eden Hazard kushindwa kutema cheche tangu alijiunga na timu hiyo mwaka 2018 akitokea Chelsea. 

 Hazard amekuwa akipambana na majeraha ya mara kwa mara yanayomfanya kushindwa kuonyesha kiwango chake kwa miezi 12 sasa tangu alipotua Santiago Bernabeu. 

Mshambuliaji Luca Jovic nae ameshindwa kung’ara tangu alipotua Madrida msimu uliopita. 

Haijafahamika ni fedha gani Zidane atakuwa nazo wakati huu majira ya joto, ingawa ukweli kwamba Madrid imeshindwa kutamba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo kumaanisha klabu hiyo imekosa pesa ambazo wangetumia kutumia kwenye ununuzi mpya. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles