23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Havertz akubali kusaini miaka mitano Chelsea

 LONDON,ENGLAND 

KIUNGO mshambuliaji wa Bayer Leverkusen ,Kai Havertz amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na wababe wa London, Chelsea, hiyo ni kulingana na ripoti kutoka gazeti la RMC Sport. 

Nyota huyo mwenye umria wa miaka 21 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliong’ara katika Ligi Kuu Ujerumani tangu alipoanza kucheza katika ligi hiyo msimu wa 2016/17 . 

Chelsea inaongoza katika mbio za kuinasa saini ya Havertz na kocha wa kikosi hicho Frank Lampard anataka kujenga upya sagu yake ya ushambiliaji akimuunganisha na wakali wengine kama Timo Werner na Hakim Ziyech msimu ujao. 

Kulingana na RMC Sport, Havertz anataka kujiunga na klabu hiyo la Magharibi mwa London na tayari ameshakubaliana nayo kuhusu maslahi binafsi ili kutua Stamford Bridge katika dirisha hili la usajili. 

 Chelsea na Leverkusen bado zinavutana katika dau la usajili na kwani klabu hiyo ya Ujermani haiku tayari kupokea chini ya Euro milioni 90. 

Mkurugenzi wa Leverkusen, Rudi Voller alisisitiza wiki hii kuwa hakutakuwa na punguzo la bei kwa nyota huyo. 

‘Tunajua mahitaji ya timu zote mbili hasa Chelsea, lakini kwetu hali ni rahisi, bado ana mktaba wa miaka miwili , kama kuna klabu inayomtaka itakubali matakwa yetu sawa,kinyume na hapo ataendelea kubaki na tunafurahia hilo,” ‘ Voller alilimbia Gazzeta dello Sport. 

Havertz amefunga mabao 17 katika mashinado yaote akiwa na Leverkusen na kuisadia kutinga hatua ya robo fainali ya katika michuano ya Europa Ligi baada ya kuitoa Rangers kwa jumla ya mabao 4-1 Alhamisi iliyopita. 

Mkali huyo anamudu kucheza maeneo mbalimbali kwenye mstari wa mbele, huku akitajwa kuwa na mchanganyiko wa staili ya uchezaji ya Michael Ballack na Mesut Ozil. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles