26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Harmonize amfokea Wolper kiana

 MWANDISHI WETU 

IMEVUJA kwamba miongoni mwa sababu zilizofanya staa wa Bongo Fleva, Harmonize aachane na Jacqueline Wolper ni usaliti alioufanya mwingizaji huyo kwa kumtaka kimapenzi, Daimond Platnumz. 

Wiki iliyopita Wolper alisikika katika moja ya mahojiano akisema sababu zilizofanya aachwe na Harmonize ni baada ya mwanamuziki huyo kupata mpenzi wa kizungu mwenye uwezo kifedha (Sarah) jambo ambapo Konde Boy amelikanusha. 

Akizungumza na maelfu ya mashabiki waliojitokea usiku wa kuamkia jana katika Uwanja wa Jamhuri kwenye tamasha la Jipoze Concert, Harmonize alisema aliumizwa na maneno ya Wolper kumwita sponsa mke wake, Sarah ambaye ni mjamzito. 

“Kuna dada mwigizaji nilimpenda sana na yeye akasema ananipenda kumbe alikuwa ananidanganya, sijawahi kusema kisa kilichofanya tuachane kwa sababu sipendi kuwasema wanawake ndio maana nikasamehe kila kitu ila mwenzangu bado ananizungumzia kwamba nilipata sponsa mzungu (Sarah) ndio maana nikamuacha. 

“Nasema kutoka moyoni, sijawahi kusema popote na mwenyewe hajui kama najua kwamba alikuwa anamwambia Diamond atamzalia mtoto wa kiume kipindi hicho Diamond alikuwa na mtoto mmoja Tiffah. Diamond alinipigia simu akaniambia mdogo wangu njoo nyumbani ukiamka tu asubuhi, Diamond alishindwa kuniambia ‘live’, ikabidi anywe pombe ndio aniambie mwanamke wako ananitaka kimapenzi,” alisema Harmonize. 

Wawili hao walikuwa wapenzi mwaka 2016 kabla ya kuachana na kila mmoja kuwa na mahusiano mengine huku wakiibua vita ya maneno kati yao kabla hawajaamua kumaliza tofauti zao na kushirikiana kwenye mambo mbalimbali, 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles