26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

‘Kuna mchezo gani kuhusu tiba ya corona’

 WASHINGTON, MAREKANI

MBIO za kupata chanjo dhidi ya covid-19 zimeshika kasi, huku mataifa kadhaa yenye nguvu kama vile Marekani, China na Uingereza yakipimana nguvu za uwezo wao wa kisayansi kwa namna yoyote ile ili kupata chanjo itakayokabili virusi vya corona.

Kwa sababu haiwezekani kubashiri ni chanjo gani itakayokuwa ya kwanza kufikia lengo la kwanza, nchi zilizoendelea sasa zimeanza kununua mamilioni ya dozi za chanjo zinazoweza kufanikiwa kutimiza vigezo vya chanjo kutoka kwa maabara tofauti kujaribu kuhakikisha wanaweza kusambaza chanjo hizo kwa watu wao.

Kwa mfano , Uingereza imesaini makubaliano na makampuni ya wasambazaji kadhaa wanaoweza kusambaza chanjo kama vile : AstraZeneca, Pfizer and BioNtech, na kampuni ya Valneva.

Marekani imefanya mikataba na makampuni kama Pfizer na BioNTech; Moderna ana Johnson & Johnson; AstraZeneca, na Novavax.

Suluhu hizi za kibinafsi, ambazo sio sehemu ya mapatano baina ya nchi, yanaweza kuelezewa kama “chanjo ya utaifa”.

 Katika mahojiano na BBC, Richard N. Haass , Rais wa Baraza la Mahusiano ya Kimataifa (CFR) na Mkurugenzi wa sera ya mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, mjumbe maalumu wa Ireland ya Kaskazini na mratibu wa mpango wa “Afghanstan ijato “, anafafanua zaidi juu kile alichomaanisha alipoandika kuwa: ‘’Kuna kisiasa, uchumi na mchezo wa kimkakati nyuma ya chanjo za corona vinavyoweza kuleta maafa “

Alisema: ‘’Tunashuhudia utaifa wa chanjo ya covid-19 ambao unaweza kuelezewa kama kinga ya utaifa’’

Serikali zimejitayarisha binafsi na sababu iko wazi. Mataifa yanakabiliwa na shinikizo ya kutoa dozi za chanjo kwa raia wao.

Mataifa yenye nguvu zaidi duniani yamesaini mikataba ya mamilioni ya dola na maabara ili kuhakikisha yanakuwa na chanjo za kutosha dhidi ya virusi vya corona

Lakini anasema tatizo ni mipango ya nchi zenye nguvu itawaacha mabilioni ya watu katika hali ya kutokuwa na uwezo wa kupata chanjo, jambo ambalo ni mzozo.

Lakini pia itakua na athari mbaya kwa serikali ambazo zitatumia chanjo za utaifa kwasababu kama kuna idadi kubwa ya watu walioambukizwa corona duniani, ikizingatiwa kwamba kuna utandawazi, ugonjwa utaendelea kusambaa.

 Kuna siasa, uchumi na mchezo wa kimkakati nyuma ya chanjo ambao matokeo yake ni mkasa.

‘’Ninaweza kuuita ushindani kwa ajili ya chanjo, sio vita. Kila mmoja anataka kupata chanjo kwanza. Baadhi kwasbabu za kisiasa, lakini wengi kwasababu za kisiasa zaidi’’ , anasema Richard Haass.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles