NA DEBORA SANJA, DODOMA
KAMATI namba tisa ya Bunge Maalumu la Katiba, imesema kuna haja ya kuongeza ibara mpya katika sura ya nne ya Rasimu ya Katiba itakayozungumzia haki za wanaume.
Mbali na hilo, wajumbe wa Bunge hilo walitaka Katiba ieleze Tanzania inaongozwa na itikadi gani kati ya ujamaa na ubepari.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kidawa Hamis Salehe, alisema wajumbe wa kamati yake walijadiliana kwa kina juu ya suala hilo.
“Wajumbe walikuwa wanatamani mambo mengi yaongezwe wakati tunajadili sura ya nne, hasa katika suala la haki za binadamu.
“Baadhi walitaka haki za wanaume nazo zitajwe kwenye Katiba kwa kile walichosema kwamba akina mama wamekuwa wakipewa upendeleo wakati wapo akina baba wanaofanyiwa ukatili na wanawake.
“Baada ya mvutano, wajumbe walipendekeza kuongezwa kwa ibara itakayozungumzia haki za wanaume,” alisema Kidawa.
Mwenyekiti huyo alisema suala jingine lililoibua mjadala walipokuwa wakijadili sura ya pili, ya tatu na ya nne, ni suala la Mahakama ya Kadhi na miiko ya uongozi wa umma.
“Kuhusu Mahakama ya Kadhi, tulikubaliana ibaki kama ilivyo katika rasimu, ibara ya 31 kwamba taasisi za kidini zipo huru kuendesha shughuli zake kwa kujifadhili zenyewe,” alisema.
Kuhusu miiko ya viongozi wa umma, alisema wajumbe walitaka kuwapo kwa adhabu kali kudhibiti wanaovunja miiko hiyo.
Akizungumzia suala la mfumo wa kisiasa wa kijamaa au kibepari kuingizwa kwenye Katiba, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Ngeleja, alisema wajumbe walitaka Katiba ieleze nchi inafuata mfumo gani.
hao wajumbe wanazidi kukosa la kufanya, nia ni kuhalalisha matumizi ya Tzs. 20 billion.