21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania waishio nje watuma ujumbe Bunge la Katiba

Samuel Sitta
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta

Na Debora Sanja, Dodoma

WATANZANIA walioko nje ya nchi, wametuma waraka maalumu kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad, alisema raia hao wameomba waraka huo ujadiliwe na wajumbe wakati huu ambapo mchakato wa kuandika Katiba unaendelea katika kamati.

“Raia walioko nje ya nchi, wametuma waraka maalumu ambao waliomba ujadiliwe ndani ya kamati kuhusiana na uraia pacha na juzi walimtuma mtaalamu wao Kadiri Singo alete waraka huo,” alisema.

Kutokana na umuhimu wa suala hilo, alisema alimuomba Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta, aruhusu waraka huo ujadiliwe ndani ya kamati na alipewa ruhusa ya kufanya hivyo.

Akizungumzia suala la uraia huo, Mwenyekiti wa Kamati namba 12, Paul Kimiti, alisema wamejadili suala hilo kwa kina na kulipitisha.

Alisema ibara hiyo ilikuwa na mvutano, hasa kwa upande wa Zanzibar ambapo baadhi ya wajumbe wamekuwa na hisia tofauti kuhusu kuruhusu uraia pacha.

“Baadhi ya wajumbe wameonyesha hofu yao, hasa kwa watu waliotorokea nje ya nchi wakati wa mapinduzi, na kwamba kuwaruhusu kuwa na uraia pacha kunaweza kuleta matatizo,” alisema.

Hata hivyo, Kimiti alisema wajumbe walipendekeza kuwapo uraia pacha kwa makubaliano ya kutungwa sheria ya kudhibiti utolewaji wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles