MKALI wa muziki wa reggae aliyewahi kuwa katika kundi la Necessary Noise la nchini Kenya, Nazizi Hirji, ameungana na msanii wa Tanzania, Zola D kwa ajili ya mafunzo ya mchezo unaotumia ngumi na mateke (Kick boxer).
Nazizi alisema amejiunga na mchezo huo ili aweke mwili wake sawa, huku akidai ataendelea kuvumilia changamoto, zikiwemo mazoezi magumu anayopata katika mafunzo ya mchezo huo.
“Baada ya kucheza mchezo huo uzito wangu umepungua, nazidisha kujituma katika mazoezi hayo kwa kuwa naamini siwezi kuujua mchezo huo bila kupata maumivu,” alisema Nazizi.