MAMA wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Wiz Khalifa, Katie Wimbush, amesema amechoshwa na tabia uvutaji wa bangi kila wakati unaofanywa na mwanawe.
Mama huyo alisema walikuwa wanavuta bangi na mwanaye tangu alipokuwa na umri mdogo hata kabla ya kuanza shule, lakini kwa sasa amezidisha matumizi ya dawa hizo kiasi cha kumkera mama huyo.
“Ilikuwa ni hali ya kawaida kabla sijaanza safari ya kwenda kazini na yeye kabla ya kuanza shule, tulikuwa tunavuta wote, lakini kwa sasa amekuwa muathirika mkubwa sana wa bangi kiasi kwamba anatumia dola 10,000 (zaidi ya milioni 20) kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya bangi,” alisema Katie.