26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TRA YATOA SOMO LA MSAMAHA WA ADHABU

DOROTH MNUBI (TSJ) NA TUNU NASSOR – DAR ES SALAAM                 |             


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema msamaha wa riba na adhabu wa asilimia 100 kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi uliotolewa kwa mwaka wa fedha 2018/19, utawasaidia wafanyabiashara kulipa kodi ya msingi na kuwapa motisha wa kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.

Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa wa mamlaka hiyo, Alfred Mregi, alisema hayo jana wakati akifungua semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya kodi kwa wafanyabiashara iliyofanyika Dar es Salaam.

Mregi alisema dhumuni la semina hiyo elekezi ni kutoa uelewa wa kutosha kwa wafanyabiashara ili waweze kuwasilisha maombi yao kwa usahihi kwa lengo la kupatiwa msamaha huo.

“Leo tumekutana mahali hapa kwa lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi, tunataka kuhahakikisha wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni wananufaika na msamaha huo unatolewa kwa asilimia 100,” alisema Mregi.

Alisema kupitia msamaha huo, wanatarajia kukusanya Sh bilioni 500.

Naye Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani, Abdul Zuberi, alisema suala la kodi halijachwa kwa TRA peke yake, bali taasisi zote za Serikali zinafanya kazi hiyo ya kuhamasisha ulipaji kodi kwa maendeleo ya Watanzania wote.

“Sasa hivi kodi za ndani zimezidi kuongezeka kutokana na uhamasishaji ambao unatoa motisha kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu,” alieleza Zuberi.

Naye mfanyabiashara kutoka Kampuni ya Super Group of Companies inayozalisha sukari ya Mtibwa na Kagera, Ibrahim Ali, alishauri TRA kutoa semina elekezi na kuongeza kuwa elimu waliyoipata imewasaidia kuelewa mambo mengi kuhusu msamaha huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles