26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

UFISADI WAITIKISA KENYA, VIGOGO WAKAMATWA

NAIROBI, KENYA


MKUU wa Shirika la Taifa la Huduma kwa Vijana (NYS), Richard Ndubai, amekamatwa.

Ndubai amekamatwa wakati uchunguzi wa upotevu wa Dola za Marekani Milioni 100 za shirika hilo ambazo ni sawa na Sh. bilioni 223 za Tanzania ukiendelea.

Kwa mujibu wa vyombo vya hahari vya hapa, Ndubai alikamatwa jana pamoja mhasibu na maafisa wanaosimamia ununuzi wa vifaa wa shirika hilo na wafanyabiashara waliohusika katika kandarasi na zabuni kadhaa.

Mkuu wa Idara ya Upelelezi, George Kinoti alikaririwa na vyomvo vya habari akisema watu 17 walikamatwa kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Aidha, Mwendesha Mashitaka Mkuu, Noordin Haji alisema mashitaka dhidi ya watuhumiwa waliotajwa katika kashfa hiyo, yataanza mara moja lakini bila kutaja majina ya washukiwa wengine.

Vituo vya Televisheni vya K24 na Citizen viliripoti kuwa, Katibu Mkuu Wizara ya Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia, Lilian Mbogo Omollo alijisalimisha polisi akiwa na mawakili wake.

Kwa wiki kadhaa sasa, vyombo vya habari nchini Kenya vimekuwa vikiripoti kuhusu wizi wa fedha za shirika hilo kupitia malipo ya zabuni za kughushi.

Kashfa hiyo na nyinginezo za karibuni ikiwamo upotecu wa Sh. bilioni 13 katika bodi ya mazao zimetia doa ahadi zilizotolewa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuwa angemaliza rushwa.

Wakosoaji wake wanamshutumu kwa kuwaonea haya maafisa wa ngazi ya juu serikalini wanaotuhumiwa kwa ufisaidi.

Wachambuzi wanasema, kushitakiwa na kufungwa kwa maafisa wakuu ndiyo njia pekee ya kukomesha ufisadi nchini  Kenya.

Tukio la kuibiwa kiasi kikubwa cha fedha za NYS si la kwanza. Mwaka 2015, NYS ilikumbwa na kashfa kama hii lakini hakuna hatua madhubiti zilichukuliwa dhidi ya watuhumiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles