25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAHITIMU JKT WATAKIWA KUANZISHA MIRADI YA MAENDELEO

Editha Karlo, Kigoma

Vijana waliopitia mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wametakiwa kurejea vijijini na kushirikiana na halmashauri zao kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha wametakiwa kuhakikisha wanawaelimisha vijana wengine kuondokana na umasikini kwa kutumia mafunzo waliyoyapata wakati wa mafunzo hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Brigedia Jenerali Marco Gaguti  ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali kwa vijana 798 wa Operesheni Mirerani waliohitimu mafunzo yao ya awali katika kambi ya Mtabila iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

“Vijana nawasihi kuondokana na mawazo ya vijana wasomi ya kutaka kuajiriwa na kuyatumia mafunzo mliyoyapata kuanzisha miradi mbalimbali kwa kujiajiri na kuwaelimisha vijana walioko mtaani,” amesema.

Brigedia Jenerali Gaguti pia amewataka vijana wote waliohitimu Mafunzo ya Operesheni Magufuli na Operasheni  nyingine kurudi katika Wilaya ya Kasulu na Buhigwe kuanzisha vikundi vya ujasiriamali  kutumia mafunzo waliyoyapata na kushirikiana na vijana walioko mtaani kuhakikisha fedha zinazotolewa na halmashauri kwaajili ya mfuko wa vijana zinatumika kuondoa umasikini.

Pamoja na mambo mengine, akizungumzia kuhusu suala la kukosekana umeme katika kambi hiyo amesema kulicheleweshwa na migogoro iliyokuwapo baina ya wakandarasi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu lakini mgogoro huo umemalizika na umeme utaanza kusambazwa hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles