Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Kundi la WCB, Raymond ‘Rayvanny’, amesema atajitahidi kuandika mashairi yatakayowafikirisha mashabiki wake ili aweze kudumu kwa muda mrefu.
Akizungumza jana, msanii huyo alisema ana imani mashairi anayoimba yamekuwa yakiwavutia mashabiki wa rika mbalimbali na kwamba, amekuwa akijitahidi kuwavutia ili kutoa nafasi ya muziki wake kukua zaidi.
“Ninachokiandika nakipitia mara mbili ili kuepusha kufungiwa au kulaumiwa kwa kufanya kazi mbaya na isiyoridhisha,” alisema Rayvanny.
Alisema anafarijika kuona nyimbo zake zinapendwa na kuimbwa hata na watoto na jambo hilo linampa faraja ya kufanya kazi bora zaidi.